Call Us
(+255) 753-956-196
Email Us
info@tagshekinah.or.tz
tagshekinah.church
Tag Shekina Church ni Kanisa la kiroho lililo chini ya Tanzania Assemblies of God ambalo lilianzishwa na Mtumishi wa Mungu Stephen Francis Mhina ambaye alianzisha Kanisa mwaka 2010 baada ya Mungu kumpa Mzigo wa kuwekeza kwenye huduma yenye kuongozwa na utukufu wa Mungu. Hapo kwanza Mtumishi wa Mungu alikuwa ni Mfanyabiashara mkubwa ambaye aliamua kumtumikia Mungu baada ya kumtendea muujiza wa kumponya mwili wake. Hata hivyo alipompokea Yesu mwaka 1992 na kutumika kanisa la TAG Magomeni na baadae mwaka 2005 alihamia Mkoani Tabora na mwaka 2010 ndipo alifungua kazi mpya ya Tag Shekinah na mpaka sasa kanisa la Mungu linakuwa kwa kasi sana na watu wengi wamekutana na Mungu kwa baraka tele; Uponyaji, Miujiza, Mafanikio na Vipawa vya roho mtakatifu.
Hasara na Umasikini Mkubwa kwa mkristo ni kuishi bila ya kuwa na utukufu wa Mungu. Ili ufanikiwe unahitaji nguvu za Mungu ili ushinde malango ya Kuzimu unahitaji kumjua Mungu. Tag Shekinah tumewekeza kuhakikisha Utukufu wa Mungu ndio maisha yetu.
Kanisa la shekina ni wazo la Serikali ya Mbinguni, Lililowekwa kwa Mtumishi wa Mungu ili kuwekeza kwenye Uamsho na Uwepo wa Mungu kwa watakatifu wake ambapo watu watakutana na Mungu katika nyanja za Kiroho na Kimwili. Mpaka sasa watu wengi wamekutana na Mungu kwa Baraka tele; Uponyaji, Miujiza, Mafanikio, Vipawa na Karama na Matokeo yake chanya ni Ukuaji na ustawi wa Kanisa kwa kasi sana.
Uwepo wa Kanisa ni uwepo wa Ufalme wa Mungu ambao hutokana na watu kuingia kupitia Kumwamini Yesu, Kufanya Utume Kwa Kuhubiri Injili Ya Kweli Ya Yesu Kristo Ili Watu Wampokee Yesu Kuwa Bwana Na Mwokozi Wao Na Hivyo Waingie Katika Familia Takatifu Na Mwisho Wawe Raia Katika Ufalme Wa Mungu. "Marko 16:15-16 Akawaambia, Enendeni Ulimwenguni Mwote, Mkaihubiri Injili Kwa Kila Kiumbe. Aaminiye Na Kubatizwa Ataokoka; Asiyeamini, Atahukumiwa." la shekina ni wazo la Serikali ya Mbinguni, Lililowekwa kwa Mtumishi wa Mungu ili kuwekeza kwenye Uamsho na Uwepo wa Mungu kwa watakatifu wake ambapo watu watakutana na Mungu katika nyanja za Kiroho na Kimwili. Mpaka sasa watu wengi wamekutana na Mungu kwa Baraka tele; Uponyaji, Miujiza, Mafanikio, Vipawa na Karama na Matokeo yake chanya ni Ukuaji na ustawi wa Kanisa kwa kasi sana.
Mchungaji Stephen Francis Mhina ni Mtanzania ambaye alizaliwa mwaka 1971 wilayani same mkoani Kilimanjaro.
Mchungaji Stephen Francis Mhina ni Mtumishi aliyempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake Mwaka 1992 katika Kanisa la Tag Magomeni – Dar es salaam ambapo alianza kuukulia wokovu kwa kuhudhuria mafundisho ya kiroho na ibada zenye nguvu za Roho Mtakatifu. Alianza kumjua Mungu hatua kwa hatua na mwaka 1998 Mungu alimjalia kufunga ndoa yake takatifu na Monica Skarion Novart ambao waliendelea kumtumikia Mungu kwa mafanikio makubwa sana ndani na nje ya kanisa wakifanyika baraka sana kwa watu wengi. Tangu mwaka 1992 mpaka mwaka 2005 alikuwa akitumika katika huduma mbali mbali za kiroho ndani na nje ya kanisa la Magomeni nchini Tanzania katika huduma za watoto, katika kufundisha neno la Mungu, Kufanya huduma za Injili, Kusimamia Idara za Vijana, watoto na Huduma za Kichungaji chini ya Ofisi ya Mchungaji.
Mwaka 2005 kwa maongozi ya Mungu aliamua kuhamia Mkoani Tabora kwa ajili ya Maisha yake ambapo alianza kuabudu kanisa la Tag Maranatha Cheyo linalosimamiwa na Mchungaji Lutengano Mwasongela. Mwaka 2006 Mungu alimpaka mafuta rasmi kwa kusimikwa kuwa mchungaji msaidizi ambapo alitumika kwa takribani miaka mitatu (3) kabla ya Mungu kusema nae kuanzisha huduma mpya kama Mchungaji mwaka 2010.Mnamo mwaka 2010 yeye na mke wake waliweza kufungua kanisa la Tag Shekinah lililoanzia nyumbani kwao Mtaa wa Mwinyi Tabora kabla ya Kumiliki Ardhi na kujenga nyumba ya Mungu. Kwa sasa wamefanikiwa kujenga nyumba ya Mungu eneo la Skanda Sekondary ambapo mpaka sasa wana washirika takribani 200.
Mtumishi wa Mungu ana Elimu ya Stashahada (Diploma) ya masomo ya Biblia na kusimamia Huduma ya kanisa ambayo aliipata katika chuo cha Central Bible College kinachomilikiwa na Kanisa la Tanzania Assemblies of God na kuhitimu mwaka 2023.
Mtumishi wa Mungu ni Mwanzilishi na Mchungaji wa kanisa la mahali pamoja la Tag Shekinah na Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Mkoani Tabora ambaye alichaguliwa mwaka 2023 (The Region Chairman Pastor of the Council of Pentecostal Churchies of Tanzania(CPCT))
Mpaka sasa Mtumishi wa Mungu na Mama Mchungaji Mungu amewabariki watoto wawili ambao ni Elisha Stephen Mhina na Aime Stephen Mhina.
Kufanya Utume Kwa Kuhubiri Injili Ya Kweli Ya Yesu Kristo Ili Watu Wampokee Yesu Kuwa Bwana Na Mwokozi Wao Na Hivyo Waongozwe na utatu Mtakatifu Tunaamini katika Utatu Mtakatifu, Neno la Mungu na wokovu kwa Mwanadamu, Hivyo tumewekeza kuhakikisha watu wanamwamini Mungu na kuongozwa na roho mtatifu huku wakimtii kwa kutekeleza maagizo na utamaduni uliohifadhiwa kwenye neno la Mungu.
Maono yetu kama kanisa ni kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, kitaifa na kimataifa wakibatizwa katika Roho Mtakatifu huku tukiwa na ibada za kiroho, mafundisho halisi na sahihi ya Neno la Mungu na hivyo kuongezeka makanisa.
Tanzania Assemblies of God (TAG) ipo kwa ajili ya kumuabudu Mungu katika Roho na kweli, katika kuuambia ulimwengu juu ya habari za Yesu na kuwapeleka waamini katika kumjua zaidi Yesu kupitia sifa, kuabudu na neno chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu."
Uaminifu Kibiblia, Uadilifu, Kuwajibika kijamii, Ushirikiano kama timu, Uvunaji kimkakati, Uwezeshaji wa uongoziUkuhani kwa waumini wote, Uwajibikaji wa usimamizi wa fedha, Ukuaji kimkakati, na Ubora."
Nembo ya kanisa itakuwa na muundo unaokaribia kufanana na ule wa makanisa mengi ya Assemblies of God duniani kote. Nembo hii itakuwa na maneno yanayosomeka “TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD”, TAG, mchoro wa msalaba na Biblia, pamoja na mchoro mwingine mdogo wa Biblia wenye alama za mwale wa moto na njiwa, pamoja na maandishi “ALL THE GOSPEL”. Nembo ya kanisa pamoja na nembo ambazo zimewahi kutumiwa na TAG hapo awali zitasajiliwa chini ya Sheria ya Alama za Biashara na Huduma ya mwaka 1986
Bendera ya kanisa itakuwa ya rangi ya bluu bahari na yenye nembo ya kanisa pamoja na maneno “JEHOVAH-NISSI”, yenye maana ya “BWANA ni Bendera yangu”. Bendera hii itakuwa sehemu ya utambulisho rasmi wa kanisa na taasisi zake popote pale, ndani na nje ya nchi.
Neno la Mungu ndio Msingi wa Imani Yetu na Kukua katika Imani
Ndio chanzo cha Maarifa na Kufanikiwa, Ni mwanga Bora
Tumeitiwa Utumishi na kuujenga mwili wa Kristo
Kumtii Mungu ndio chanzo cha Baraka kwa Waamini
Huu ndio mwito wa kufanya kwa Dunia yaani wokovu kwa wote
Hakuna lisilowezekana kwa Mungu kwa Kusali na Kuomba
Tunamgusa Mungu kwa kuigusa Jamii kwa kusaidia
Kanisa tunaamini ujio wa Yesu mara ya Pili kutwaa Kanisa
Mungu huwatumia kutimiza Malengo
Tumeitwa Kubariki
Tunawasiliana na Mungu
Tunaweza kumtumikia Mungu kwa Viwango
Ndio Kanisa la Leo na Kesho
Ni Utajiri na Hazina kuu
Ndio Kanisa Lenye Nguvu
Ni kumgusa Mungu zaidi
Ndio chanzo cha Baraka za Ibrahimu