Kuhusu Idara ya Uanafunzi (Discipleship)
Sisi ni Wanafuzi wa Yesu
Idara hii ilizaliwa rasmi mwaka 2008 na ikakabidhiwa kama ofisi rasmi na Mchungaji David mwakajinga tarehe 12/12/2008. Jambo hili lilikuwa ni utekelezaji wa matakwa ya katiba ya Tanzania Assemblies of God iliyokuwa imeagiza kuwepo na Idara hii. Vile vile Idara hii ilianzishwa kama chombo cha utekelezaji wa mpango mkakati wa kwanza wa kanisa chini ya Askofu mkuu mpya na wa awamu ya tatu ya maaskofu watanzania, Dktr, Barnabas Mtokambali. Viongozi waanzilishi walikua ni Rev. Elingarami Munisi aliyekua Mkurugenzi Mkuu, Rev, profesa Joseph Kimeme aliyekua Makamu wake, Rev. Moses Magembe aliyekuwa Katibu Mkuu wa Idara na huu ndio ukawa mwanzo wa Idara hii.";
Shekinah Intercessory Temple