Kuhusu Idara ya Muziki na Uimbaji
Idara ya Muziki na uimbaji kitaifa ilianzishwa rasmi mwezi septemba mwaka 2021. Kama kitengo cha muziki na uimbaji cha kusimamia mchakato wa uanzishwaji wa wa Idara hii wakati wa uongozi wa Askofu Mkuu wa TAG Dr.Rev. Barnabas Mtokambali. Uanzishwaji huu ulitoka na lengo mkakati (B4) la Miaka Kumi na tatu ya Moto wa Uamsho. Eneo la huduma ya Idara ya DMS litakuwa nchi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tanzania Bara na Zanzibar. Aidha, kwa mwongozo wa Ofisi Kuu ya TAG, idara hii itaweza kufanya kazi nje ya mipaka ya Tanzania. Jina la Idara ni “Idara ya Muziki na Uimbaji”, kwa Kiingereza “Department of Music and Singing” kwa kifupi “DMS”.Andiko la Idara ya DMS litakuwa ni Yohana 4:24 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Shekinah Intercessory Temple