Ijue Idara ya Maombi TAG
Idara ya Maombi Kitaifa ilianzishwa Rasmi mwezi septemba mwaka 2021, wakati wa uongozi wa askofu Mkuu Dr. Rev. Barnabas Mtokambali, kutokana na Lengo Mkakati (A2) la Miaka 13 ya Moto wa Uamsho, Unatoa ufafanuzi kwamba idara ya Maombi imeanzishwa na Viongozi wa Idara wamepatikana. Lengo Kuu la Idara hii ni kuona kanisa lote tumeshika silaha hii kubwa ya Maombi ambayo ndio itakua Kichocheo kikubwa cha kusababisha uamsho wa kweli utokee.
Shekinah Intercessory Temple