• We are Located near Skanda Secondary School, Mwinyi Street - Tabora

Christ's Ambassadors (CA's);

Sisi ni Wajumbe Wajumbe wa Kristo

Jina la Idara ni Tanzania Assemblies of God - Christ's Ambassadors (CA's); Yaani ikiwa na maana ya Vijana mabalozi wa Kristo. 'Kimsingi ni Idara ya Vijana'.Idara ya Vijana (CAs) ni moja kati ya idara 11 za kanisa zuri la kipentekoste Tanzania Assemblies of God. Vijana walioko katika kanisa la TAG ni wajumbe wa idara. Idara hii ina makusudi makuu 7 ambayo ni dira ya utumishi wake katika kuipeleka mbele idara na kuwafanya wajumbe wa Kristo kutimiza wajibu wao wa msingi kwa Bwana.Makusudi hayo ni yafuatayo Kushuhudia, Kujifunza Neno, Kuabudu, Kutumika, Ushirika, Kujifunza Uongozi, na Kutekeleza dira ya maendeleo ya Kanisa la TAG.Idara ya Vijana ya kanisa la Tanzania Assemblies of God, yaani CAs haikuchipuka na kuwa idara kamili mara moja. Historia inaonyesha shughuli za idara ya Vijana zilikuwepo makanisani lakini hakukuwa na mfumo rasmi wa uendeshaji. Kimsingi Vijana wapo kutekeleza mwito mkuu wa "Mathayo 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu";

MaonoKuandaa Vijana wenye Sifa Hizi:-

  • Waliojaa Roho Mtakatifu kikamilifu
  • Waliohamasika Kihuduma
  • Wenye uwezo wa kuvuna roho zilizopotea
  • Viongozi bora wa Kesho na waaminifu
  • Kuandaa watumishi wawajibikaji
  • Kuandaa Jamii iliyofanikiwa

MaadiliMakusudi ya Idara ni:-

  • Kushuhudia
  • Mafunzo kwa ajili ya Uinjilisti kwa Mbinu
  • Vijana wenye nguvu za Mungu
  • Vijana washindi wa dhambi
  • Vijana wenye manufaa kwa kanisa
  • Vijana wenye manufaa kwa Jamii na Taifa

CA'S

"IDARA YA VIJANA"


Kwa kuwa sisi wana vijana tu wajumbe kwa ajili ya Kristo tunaamua kwa dhati kutangaza Neno la Mungu ulimwenguni.

PCF

"PASTOR'S CHILDREN FELLOWSHIP"


Huu ni ushirika wa watoto wa wachungaji unaojulikana kama Pastors’ Children Fellowship wenye lengo la kuwaunganisha.

SHULE

"EBENEZER SEMINAL SCHOOL"


Shule ya sekondari Ebenezer ni shule ya Kiseminari inayomilikiwa na kanisa la TAG chini ya usimamizi wa Idara ya Vijana.