• We are Located near Skanda Secondary School, Mwinyi Street - Tabora

Historia ya Tanzania Assemblies of God

Tanzania Assemblies of God ni kanisa lililotokana na uamsho mkubwa ulioanza huko mtaa wa Azusa, California nchini Marekani, mwanzoni mwa karne ya 20. Paul Deer ambaye awali alikuja kama mmishonari wa kujitegemea, na alianzisha Kanisa la Pentecoste Holiness Association (PHA) mnamo mwaka 1928 ambapo ibada ya kwanza hasa ya Kanisa hilo ilianza mapema mwaka 1929 huko Igale katika Wilaya ya Mbalizi mkoani Mbeya. Mnamo mwaka 1938 Derr alirejea Marekani na mwaka uliofuata 1939 alijiunga na Kanisa la Assemblies of God, na hivyo kuikabidhi kazi iliyokuwa imeanzishwa Tanzania (wakati huo ikiitwa Tanganyika) mikononi mwa Genenral Council ya Assemblies of God Marekani. Na kuuomba uongozi huo wampeleke Mmissionari kwenye kazi hiyo kuilea wakati yeye akiwa likizoni.

Historia inatuonesha kuwa katika miaka ya mwanzo kanisa lilisimamiwa na wamishonari wa kimarekani pamoja na wachungaji wa kiafrika wakati huo {Yohana Mpayo [Marehemu] na Petros) waliokuwa maaskofu chini ya Assemblies of God Mission. Kanisa liliendelea kuongozwa katika mfumo huo hadi mwaka 1967. Kanisa la kwanza kabisa la TAG lilikuwapo pale Igale wilaya ya Mbalizi mkoani Mbeya. Ni mwaka huo wa 1967, uongozi wa Assemblies of God Mission, uliamua kulikabidhi kanisa kwa uongozi wa wenyeji na Mchungaji Immanuel Lazaro, alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza mtanzania wa kuongoza Tanzania Assemblies of God (TAG). Kanisa hili liiingia hapa nchini kama matokeo ya uamsho mkubwa wa Kipentekoste uliotokea kule Azuza Marekani. Hivyo lengo kuu la kuanzishwa kwa kanisa ni kuwafikia wenye dhambi kwa injili iliyo hai, iletayo wokovu na kuleta uamsho mkubwa wa Bwana wetu Yesu Kristo hapa nchini. ili kutimiza lengo hilo ilikuwa lazima watendakazi shambani mwa Bwana waandaliwe tangu utoto.

Kuingia Nchini Tanzania

Kwa Ufupi, Mmishonari Paul Deer aliingia nchini na kuanzisha kazi ya Mungu mwaka 1928 kama mmishenari binafsi. Takwimu za kihistoria zinatuonesha kuwa mtumishi huyu aliikabidhi huduma yake aliyoainzisha Tanganyika kwa Assemblies of God (AG) kule Marekani mwaka 1939. Hapo ndipo hesabu za umri wa kanisa letu hapa nchini zinapoanzia, hivyo kutupa uhalali wa kusherehekea miaka 75, ya uhai wa Tanzania Assemblies of God Mwaka huu wa 2014. Historia inatuonesha kuwa katika miaka ya mwanzo kanisa lilisimamiwa wamishenari wa kimarekani, wachungaji wa kiafrika wakati huo, Yohana Mpayo (Marehemu) na Petros, walikuwa maaskofu chini ya Assemblies of God Mission. Kanisa liliendelea kuongozwa katika mfumo huo hadi mwaka 1967. Kanisa la kwanza kabisa la TAG lilikuwapo pale Igale, Wilaya ya Mbalizi, Mkoa wa Mbeya.

Ni mwaka huo wa 1967, uongozi wa Assemblies of God Mission, uliamua kulikabidhi kanisa kwa uongozi wa wenyeji na Mchungaji Immanuel Lazaro aliyechaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza mtanzania wa ili kuongoza Tanzania Assemblies of God (TAG). Kanisa hili liliingia hapa nchini kama matokeo ya uamsho mkubwa wa Kipentekoste uliotokea kule Azuza Marekani. Hivyo lengo kuu la kuanzishwa kwa kanisa ni kuwafikia wenye dhambi kwa injili iliyo hai, iletayo wokovu na kuleta uamsho mkubwa wa Bwana wetu Yesu Kristo hapa nchini. Ili kutimiza lengo hilo ilikuwa lazima watendakazi shambani mwa bwana waandaliwe tangu utoto wao.

Usajiri na Uanzishwaji wa Kanisa Hili Tanzania

Tanzania Assemblies of God (TAG) ilisajiliwa tarehe 21/10/1981 chini ya sheria ya Societies Ordinance ya mwaka 1954 na kupewa namba ya usajili SO. 6246. Tanzania Assemblies of God (TAG) ni Taasisi iliyosajiliwa tarehe 21/10/1981 chini ya sheria ya Societies Ordinance ya mwaka 1954 ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzaniana kupewa namba ya usajili SO.6246 Kama shirika lisilo la Faida. Ni dhehebu la Kikristo lisilo na Faida ambalo linajikita katika kuhubiri Injili ya Kweli ya Bwana Yesu Kristo kwa kutimiza Kusudi la Kanisa ambalo ni Uinjilisti, Ushirika, Ibada, Ukomavu wa Kiroho na Huduma kwa ujumla. Tuna Ukweli wa Msingi ambao sisi kama kanisa la pentekoste tunaamini na kuishi kwa msaada wa Roho Mtakatifu na jina kuu la Yesu Kristo. Pamoja na kuwekeza sana katika Huduma za kiroho, Kwa sasa Kanisa limefahamu umuhimu wa kuigusa jamii hivyo linajishughulisha na Miradi kadhaa inayoigusa Jamii.

Shina la Kanisa hili ni jijini Mbeya na baade kuweka Ofisi za makao makuu kitaifa kuwa Dar es salaam(Tag - Upanga Christian Centre) lakini kutokana na kuunga mkono Juhudi za Serikali na ndoto za aliyekuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere za Kuhamishia Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma, Mnamo tarehe 01/11/2021 Makao Makuu ya kanisa letu yalihamishiwa Dodoma ambapo na huduma zote za Kitaasisi kitaifa zinatolewa jijini Dodoma.

project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image

Muonekano wa jengo la ofisi ya Makao Makuu ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) ambalo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilizindua jijini Dodoma, Agosti 12, 2022. Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Waziri Mkuu alipozungumza akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Uzinduzi wa jengo la ofisi ya Makao Makuu jijini Dodoma.



Historia ya Watumishi wa Mungu Tanzania


project-slider-image

TAG Church Tanzania

Executive Team

team-img

Dr. B. Mtokambali

Bishop Tanzania

team-img

Dr. Magnus Mhiche

Assistant Bishop Tanzania

team-img

Rev Joseph Marwa

General Secretary

team-img

Rev Nimrod Swai

Chief Accountant

Matukio ya Kitaifa Pichani

service-image

Makao Makuu ya Tag

Hii ni Ofisi iliyofunguliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa Jijini Dodoma.

Learn more
service-image

Makao Makuu ya Tag

Hii ni sehemu ndogo ya Watu waliohudhuliwa uzinduzi wa Ofisi ya Tag Makuu jijini Dodoma.

Learn more
service-image

Mkutano Mkuu wa Tag

Maelfu ya watumishi walihudhuria Ufunguzi huo tarehe 08-12/09/2022, jijini Dodoma.

Learn more
service-image

Makao Makuu ya Tag

Picha ya Pamoja kati ya Askofu Mkuu wa Tag na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Jijini Dodoma.

Learn more
service-image

Kuwekwa Wakfu

Mhazini Mkuu Mch Nimrodi Swai akiwekwa Wakfu na Askofu Mkuu Jijini Dar es salaam (Picha za Maktaba ya Tag)

Learn more
service-image

Mfumo wa Bezaleli

Picha za Kumbukumbu kwenye Uzinduzi wa Mfumo wa bezaleli (Picha za Maktaba ya Tag)

Learn more