• We are Located near Skanda Secondary School, Mwinyi Street - Tabora

Huduma za Kiroho

Tag Shekina Church ni Kanisa la kiroho lililo chini ya Tanzania Assemblies of God ambalo lilianzishwa na Mtumishi wa Mungu Stephen Francis Mhina ambaye alianzisha Kanisa mwaka 2010 kwa Mungu kumpa Mzigo wa kuwekeza kwenye huduma yenye kuongozwa na utukufu wa Mungu kwa sababu anaamini Kanisa bila ya utukufu wa Mungu ni sawa na kampuni ya biashara. Kanisa bila ya kuwa na utukufu wa Mungu ni sawa na kutokuwa na Uamsho katikati yao. Tangu kanisa hili lianze limekuwa linakuwa kwa kasi sana, Mpaka sasa watu wengi wamekutana na Mungu kwa baraka tele; Uponyaji, Miujiza, Mafanikio na Vipawa vya roho mtakatifu.

Shekina au Shekhinah / schechinah, Ni neno la kiyahudi linalomaanisha, “kutua” au “kuweka makao” au “makazi” ya uwepo wa Mungu duniani. Hivyo utukufu wa Shekina maana yake ni kujifunua kwa uwepo wa Mungu kwa dhahiri duniani, ambapo kuonekana kwake kunaweza kuchukua mfumo wa vitu mbalimbali vya asili , kama vile moto, wingu,moshi,mwanga, kijiti kinachoteketea n.k. Mara ya kwanza utukufu wa Shekina kuonekana ilikuwa ni siku ile wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Misri, kuelekea Jangwani walipokuwa pale Sukothi, siku hiyo ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kuuona uwepo wa Mungu dhahiri katika wingu na nguzo ya moto (Kutoka 13:20-22. Kanisa ni Taasisi inayowakilisha Ufalme wa Mungu duniani, hivyo ili Mungu aitembelee dunia anapitia kanisani akiwa ndani ya utukufu wake .Hivyo kwa kifupi tunaweza kusema utukufu wa shekina tulionao sasa ni YESU KRISTO na roho mtakatifu. Na kila mmoja wetu ameweza kumwona Mungu zaidi hata ya wale waliotokewa katika nguzo ya moto,ikiwa tu atakubali kuingia katika neema yake.

Mwito wa Mchungaji kwa kanisa ni; Kukuchunga na kukujenga uwe mkristo Imara mwenye Mahusiano binafsi na Mungu ama kuwa na ukaribu na Mungu ya kwamba Mungu anayemjua Mchungaji wako uweze kumjua ikiwezekana zaidi ya viwango vyake (vyangu) na hivyo ukishamjua Mungu na kuwa na mahusiano ya karibu hakika atakusaidia kibinafsi. Mkristo asiye na mahusiano na Mungu akipata makwazo hawezi mtegemea Mungu na ataanguka; Mchungaji hupenda wakristo wasiweke Tumaini kwake bali waamini katika kumtegemea Mungu na wawe nae kikamilifu nae atajifunua katika maisha yao.

Mch Stephen Francis MhinaFounder
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image
project-slider-image

What Makes Us Different?

Jamii ya wakristo wengi wa sasa wameendelea kuishi kwa maisha ya mashaka na kutokufikia lengo lao na la Mungu pia kwamba wafanikiwe. Matokeo wamejikuta wanaangukia kwenye Imani potofu ambazo zimewatesa na kuwaletea majanga na umasikini mkubwa kwa kuwapa vyakula visivyofaa, Tag shekinah Church tumewekeza katika:-

  • Ushirika wa Mtu na Mungu ni wa msingi.
  • Maisha Matakatifu na Kumhofu Mungu.
  • Kuliishi neno la Mungu siku zote.
  • Kuwaandaa watumishi wa leo na kesho.

what you should know?

Tunaamini kwa Mungu wa Kweli aliyefunuliwa kupitia neno lake Takatifu.

Maono yetu kama kanisa ni kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, kitaifa na kimataifa wakibatizwa katika Roho Mtakatifu huku tukiwa na ibada za kiroho, mafundisho halisi na sahihi ya neno la Mungu na hivyo kuongezeka makanisa.

Tanzania Assemblies of God (TAG) ipo kwa ajili ya kumuabudu Mungu katika Roho na kweli, katika kuuambia ulimwengu juu ya habari za Yesu na kuwapeleka waamini katika kumjua zaidi Yesu kupitia sifa, kuabudu na neno chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.

Uaminifu Kibiblia, Uadilifu, Kuwajibika kijamii, Ushirikiano kama timu, Uvunaji kimkakati, Uwezeshaji wa uongoziUkuhani kwa waumini wote, Uwajibikaji wa usimamizi wa fedha, Ukuaji kimkakati, na Ubora.

Umependezwa na Huduma yetu?