• We are Located near Skanda Secondary School, Mwinyi Street - Tabora

Kuhusu Idara ya CASFETA


CASFETA ni jumuiya ya wanafunzi walio mabalozi wa Kristo Tanzania yenye malengo tangu kuanzishwa kwake. Ushirika huu ni hitaji la wanafunzi walioko shule za sekondari na vyuoni kumuabudu Mungu kulingana na imani ya Kipentekoste. CASFETA ilianzishwa mwaka 1992. Wazo lake lilianzia kwa viongozi wa Idara ya vijana wa TAG, yaani Christ’s Ambassadors (CAs). Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CAs, mchungaji Uswege Mwakisyala alikuwa ndiye Mwenyekiti wa kamati ya watu watatu. Askofu Mkuu wa wakati huo Mchungaji Ranwel Mwenisongole alijibu kwa barua yake ya tarehe 8/10/1992, kuikubali huduma hiyo ianzishwe na kusimamiwa na idara ya Vijana CAs. CASFETA ilipata Mkurugenzi mpya 2008, Mch. Dkt. Huruma Nkone ambaye katika uongozi wake iliendelea kukua na kuzifikia shule, vyuo na vyuo vikuu vingi hapa nchini Tanzania, ambapo hadi kufikia mwaka 2020 kumekuwa na matawi zaidi ya elfu mbili mia tisa (2,900) nchini kote.

MaonoKuwa kizazi kinachotembea katika nguvu za Roho Mtakatifu na kuubadilisha ulimwengu kwa Neno la Mungu. Kesho ya kanisa la TAG ni kuwaandaa Vijana wenye Maarifa ya dunia na Mungu kuathiri dunia kwa maendeleo.

MakusudiKuwafundisha wanafunzi kuepukana na matendo yanayoharibu jamii kama vile; Utoaji mimba, Ulevi, Utumiaji madawa ya kulevya, Ushoga, Usagaji, Ubakaji, pamoja na matendo mengine yote maovu.