Fahamu Dhana ya Uongozi kwa Ujumla wake
Hitaji kubwa la nyakati zote tangu vizazi na vizazi, katika watu wa kada zote, jamaa, Taifa, Mataifa, Taasisi na Mashirika ya dini ni kupata viongozi wenye sifa na uwezo wa kuwaongoza wengine, pia wenye uwezo na hekima katika kuwaunganisha watu ili kuwafanya kuwa wamoja katika kutumia karama, vipawa, talanta, huduma na rasilimali walizonazo kwa manufaa ya maendeleo yao. Pia waweze kufikia na kukamilisha jambo/malengo na mipango yao waliyokusudia.
Asili yote ya Uongozi na Utawala, unatokana na Mungu mwenyewe, Mwanzo 1:26-27. Alipanga kila mwanadamu awe mtawala, ila kusudi lake liliharibiwa na dhambi, Mwanzo 3:1-10.Dhambi ya Mwanadamu ilichelewesha Mpango wa Mungu, Kutoka 32:1-6 linganisha na Kut 19:5-6. Hivyo Mpango wa Mungu ulitimizwa kupitia kifo cha Kristo alipokuja hapa duniani 1Pet 2:5-9. Uongozi na Utawala ni Vitu viwili tofauti ndani ya Kanisa, Makanisa mengi hayana Uongozi bali yana Utawala. Wapo wanaopenda kwa viongozi katika Jamii lakini hawana sifa na wapo wasiopenda kuwa viongozi bali wana sifa ya kuwa viongozi. Mojawapo ya matatizo na migogoro inayopelekea kanisa kutokupiga hatua leo ni pamoja na kutokuongozwa sawa sawa yaani leadership and style.
Kutoka 18:21 ''Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;''
Fahamu maana ya Uongozi/Utawala
[1] Uongozi ni hali/tendo la kuongoza. Ni hali ya kutangulia mbele, kusimamia, kulinda na kuelekeza watu njia au mwelekeo wa kuuendea au kufikia malengo Fulani.Kiongozi ni mtu Yule ajuaye njia na yale apaswayo kupita nayo na kuzingatia katika njia hiyo.Ni mtu Yule ajuaye mwelekeo wa jambo hilo au malengo hayo na anauwezo wa kuwatangulia na kuwavutia (shawishi) wengine wamfuate.
[2] Uongozi ni Utumishi siyo Ubwana, bali ni kuwa kielelezo kwa kundi 1Pet 5:3 1Tim 1:16. Uongozi ni ushawishi, ni uwezo wa mtu mmoja kuwashawishi wengine waweze kufuata Uongozi wake. Uongozi wa Kiroho unaweza kutimizwa na watu wa kiroho pekee. Neno Uongozi linatokana na neno Kuongoza, ni ile hali ya mtu kuwatangulia wengine na kisha wengine hufuata nyuma.
[3] Utawala ni ni kule kusimamia, kumiliki, kunyenyekesha, kuamuru na kutiisha. Kwa hiyo kutawala ni kutumia Uwezo au Nguvu au daraka ulilonalo kuamuru na kutiisha.1.Uongozi ni hali/tendo la kuongoza. Ni hali ya kutangulia mbele, kusimamia, kulinda na kuelekeza watu njia au mwelekeo wa kuuendea au kufikia malengo Fulani.Kiongozi ni mtu Yule ajuaye njia na yale apaswayo kupita nayo na kuzingatia katika njia hiyo. Ni mtu Yule ajuaye mwelekeo wa jambo hilo au malengo hayo na anauwezo wa kuwatangulia na kuwavutia (shawishi) wengine wamfuate. Kiongozi Mzuri ni yule anayeandaliwa mfano:-
(a) Mungu alimuandaa Ibrahimu na kumwita ili kuanzisha Taifa
(b) Akamwandaa Musa ili kulitoa Taifa hilo Utumwani - Kut.3:2-14
(c) Akamwandaa Joshua kuliongoza Taifa hilo kuteka nyara, kupigana vita na kuliingiza Kanani - Yoshu 1: 1 - 9.
(d) Mungu alitumia wanaume na wanawake katika kufikia malengo yake kama vile Nabii Debora - Amuzi 4:4, Esta 7: 3 - 6 n.k.
(e) Pia Mungu aliwaongoza na kuwaelekeza waamuzi na wafalme katika kulisimamia kundi lake (watu) la Mungu, pia aliwatumia Manabii ili kuwaonya na kuwasahihisha watu wa Mungu;
(f) Na hatimaye alimtuma mwanaye wa pekee mpendwa Yesu Kristo kuja kufa na kufufuka kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu kutoka katika utumwa wa dhambi - Yoh. 3:16, Math. 1:21.
(g) Yesu naye alipoondoka akamtuma Roho Mtakatifu ili atuongoze salama - Yoh. 14: 16,26, Rumi. 8:14
Mchungaji Stephen Francis Mhina Anaamini kwamba, Kanisa na Jamii haviwezi kufanya maendeleo makubwa bila ya kuowa na uongozi bora, Tag Shekinah imejikita kuhakikisha viongozi wa idara wanaochaguliwa wanakuwa na sifa na pia baadae wanaandaliwa kuwa bora kwa ajili ya kulifaa kanisa, Jamii na Taifa. Kanisa huandaa seminal na mafunzo maalumu katika kuhakikisha wanaongoza kwa ustawi. Ezekieli 22:30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.
Shekinah Intercessory Temple