• We are Located near Skanda Secondary School, Mwinyi Street - Tabora

Kuhusu Idara ya Wanawake


Idara ya Wanawake imeanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 20 sehemu ya 7 ya katiba ya Tanzania Assemblies of God. Hivyo kutokana na msingi huo Idara ya WWK imeandaa taratibu na muongozo wa Idara ya WWK kwa msingi wa kuongoza na kusimamia shughuli zote za Idara hii.

DhimaKuwa na wanawake wa kanisa la TAG mbao ni jeshi halisi la Bwana Yesu, walio jaa nguvu za roho mtakatifu, wenye kasi ya kueneza Injili katika jamii zao, Kuigusa jamii inayowazunguka kwa kusaidia kwa mujibu wa kanuni za kibiblia. Pia idara ya WWK ipo kwaajili ya kuwaunganisha wanawake wote wa kanisa la TAG kitaifa na kanisa la mahali pamoja kwa kuwakuza kiroho, kuwapandikiza maono na mzigo wa kutumika na kutoa mafundisho yatakayowawezesha wanawake kutimiza agizo kuu la Bwana.

MaadiliUaminifu kwa Biblia kwa kuishi mafundisho yake. Kuwajibika kijamii tukidhihirisha upendo na Haki ya Mungu katika maneno na matendo, Kufanya pamoja kama timu kwa kua na mahusiaono mema baina yetu na watu wengine. Kuvuna Kimkakati, Kuwawezesha viongozi, ukua kimkakati, Utawala wa fedha unaowajibika na Kuwajibika katika kicho cha Kristo. Mwanamke Mcha Mungu ndiye anaweza kumtumikia Mungu kwa ufanisi Mkubwa hivyo inampasa mwanamke kuwa mwenye maadili ya Mungu na Utakatifu kimwili na kiroho.