Ifahamu Idara ya CMF
Kuwepo kwa Idara hii kunahamasisha wanaushirika huu kufanya uamuzi wa dhati kuleta mabadiliko katika maisha yao na jamii yote. Maono ya kuwako kwa Ushirika wa Wanaume Wakristo, yaani Christian Men’s Fellowship (CMF) una historia ndefu katika TAG. Kwanza, wazo lilianza kama shauku ya uongozi wa Kanisa kitaifa, Pili, ilitokana na hitaji la wanaume wenyewe, na vilevile lilikuwa ombi la muda mrefu kutoka kwa Idara ya Wanawake Watumishi wa Kristo (W.W.K) wa kanisa letu. Mwaka 2008, wakati wa awamu ya tatu ya uongozi wa kanisa chini ya Askofu Dr. Barnabas Mtokambali, TAG ilitengeneza Dira ya Maendeleo ya Kanisa ya utekelezaji wa miaka kumi ya mavuno. Katika Eneo C linalosema “Inua viwango vya Ibada ya binafsi na pamoja”, kipengele cha C4:5-kina mkakati unaosema, “Anzisha Idara ya Wanaume”.
Shekinah Intercessory Temple