Ifahamu Idara ya Elimu
Kanisa la Tanzania Asssemblies of God lilipoanza mwaka 1939 halikua na chuo chochote cha Biblia wala mafunzo yeyote rasmi yaliyotumika kuandaa Watumishi. wamishenali walihubiri Injili na watu waliokoka na miongoni mwa watu waliookoka waliosikia wito wa Uwalithibitishwa na viongozi na kuingia shambani na kumvunia Bwana mavuno. Baadaye ikaonekana kuna uhitaji wa mafunzo rasmi ya kuwaandaa Watumishi kwa ajili ya kulifikia taifa kwa Injili ya Bwana Yesu Kristo. Ndipo mnamo mwaka 1980 kamati kuu ya wakati huo chini ya Uongozi wa Mchungaji Emmanueli Lazaro (Askofu Mkuu), Mchungaji Enos Kameta (Makamu Askofu Mkuu) na Mchungaji Solomoni Mwagisa (katibu Mkuu) walikaa na kushauriana na WWamishenari waliokuwepo wakati huo na kwa pamoja walikubaliana kuwepo kwa Idara ya Elimu na huo ndio ukawa mwanzo wa Idara hii.
Idara ya Elimu ni mojawapo ya Idara kumi na moja za Kanisa la Tanzania Assemblies of God, iliyoanzishwa kwa ajili ya kufanikisha maono na malengo yake. Kusudi la kuwepo kwa Idara ni kupanga, kuratibu, na kusimamia utekelezaji ili kuwa na watumishi waliondaliwa vema kiroho na kitaaluma, wenye kuakisi tabia na mtazamo wa Yesu katika maisha na huduma. Idara inatoa mafunzo kwa watumishi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God na Madhehebu mbalimbali ya Kipentekoste tunayokubaliana nayo kiimani ndani na nje ya nchi.Idara ya Elimu ina Vyuo vya Biblia tisa. Vyuo vya bweni saba, kimoja cha kutwa, na kimoja huria. Ili kuharakisha kazi ya kuivuna Tanzania. Lengo kuu ni Kuratibu mafunzo yatolewayo katika Vyuo vya Biblia, Vyuo vya Kupanda Makanisa na Mafunzo Endelevu ili kutoa elimu bora kwa lengo la kuwa na watumishi wenye uwezo na maadili ya kibiblia. Kuandaa mtaala wenye sifa zinazohakikisha kwamba elimu inayotolewa inakidhi hitaji la Kanisa la TAG na aina ya cheti kinachotolewa kwa mhitimu.

Shekinah Intercessory Temple