Fahamu Maana ya Kanisa na Jamii
Jamii ni kundi la watu wanaoshiriki katika uhusiano endelevu wa kijamii, au kundi pana la kijamii linalochukua eneo lile lile la kijamii ambalo kwa kawaida linawekwa wazi kwa nguvu sawa za kisiasa na viwango vya kitamaduni ambavyo vinatawala. uwepo wa jamii kwa sera moja huwezesha serikali kutawala kiurahisi. Kanisa ni Muunganiko wa watu wa jamii moja wanaomwamini Mungu kwa lengo la kuishi maisha ya uchaji wa Mungu wakati wanafanya shughuli mbali mbali za maendeleo.
Maendeleo ya jamii ni mchakato wa kujenga uwezo wa jamii endelevu, inayojiamini na yenye uwezo wa kujituma na kushiriki kwa misingi ya usawa na kuheshimiana, katika kubaini mahitaji yao. Aidha kubuni, kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya kujiletea maendeleo kwa kutumia kikamilifu raslimali za ndani na nje. Jamii hazifanani na hivyo matatizo ya jamii pia hutofanutiana. Jamii hutofautiana kutokana na mila, imani, desturi, maadili na historia inayorithishwa kutoka kikazi kimoja hadi kingine na mazingira wanamoishi na kazi zinazowezesha kujikimu. Vigezo hivyo vinaweza kuwa vichocheo au vikwazo katika kuleta maendeleo.
Ustawi wa Jamii ni mchakato wa kujenga jamii kimaadili ili istawi kwa kumsaidia mtu mmoja mmoja mwenye tatizo la kifamilia ambalo linaweza kumsababishia madhara (kijamii, kisaikolojia na kiuchumi) au kikundi cha watu wenye tatizo linalofanana.
Mambo yanayofanyika na Jamii ya Watu wa Mungu
- Kuunganisha nguvu za jamii bila kujali itikadi ili kuondoa fikra tegemezi.
- Kutoa elimu kwa vikundi vya kijamii kuhusu uchumi na ili kuona namna ya kupamabana na umasikini.
- Kufanya tafiti shirikishi za kijamii na kiuchumi ili kubaini fursa na vikwazo katika kujiletea maendeleo.
- Kuimarisha haki na demokrasia ili kuongeza kasi ya maendeleo ya watu.
Mchungaji Stephen Francis Mhina Anaamini kwamba, Kanisa na Jamii hauwezi kuvitenganisha kwa sababu Mpango wa Mungu Kuanzisha Kanisa lake ni ili aweze kuifikia Jamii. Hivyo Tag Shekinah Tuna miradi mbali mbali katika Jamii katika kuona tunaiunganisha jamii katika shughuli za maendeleo na kuongeza Hofu ya Mungu katika Jamii.
Shekinah Intercessory Temple