• We are Located near Skanda Secondary School, Mwinyi Street - Tabora

Ifahamu Idara ya Watoto ya Tag Shekinah


Katika vitu ambavyo ni vya muhimu na vya kuzingatia kwa wazazi au walezi, ni uangalizi wa hali ya juu wa watoto tangu udogo wao, kwa sababu, ukisha haribu misingi ya malezi ya mtoto tokea akiwa mdogo, pindi atakapo kuja kuwa kijana au mtu mzima, anakua ni mzigo na mwiba katika jamii, Taifa kwa ujumla, na kwa mama yake.

Mambo ya Msingi Kuhusu Watoto


Mathayo 19:14 Lakini Yesu akasema, waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.

Kwanza kabisa, Jambo la kwanza kwa wewe mzazi au mlezi, unatakiwa uwe ndani ya Kristo, yaani umeshatubu dhambi zako kwa kumwamini Yesu Kristo na kubatizwa katika ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, na kupokea Roho Mtakatifu ambaye ni muhuri wa Mungu (Waefeso 4:30).Na ukisha kidhi hivyo vigezo, basi yafuatayo ni ya kuzingatia juu ya mtoto wako.

1. Mweke mtoto wako wakfu mbele za Bwana madhabahuni kanisani

kumuweka wakfu mtoto madhabahuni kanisani ni kumbariki mtoto na kufungua njia ya kumwamini Mungu tangu akiwa na mwaka sifuri au zaidi, na hii itampa mtoto nafasi ya Mungu kutembea nae katika udogo huo huo, na pia, hapa pana uhitaji wa kuelewa vizuri zaidi tunapo sema, “kumweka mtoto wakfu”.haina maana kuwa mtoto anaupokea wokovu bali maana yake ni kwamba, kumwekea ulinzi wa ki-Mungu katika ukuaji wake na Baraka kutoka kwa Bwana.

Marko 10:16 Akawakumbatia, Akaweka mikono yake juu yao, Akawabarikia.

2. Kumwombea mtoto na kwenda nae nae ibadani

Licha ya kumweka wakfu kwa Bwana, unapaswa pia kuwaombea watoto wako mbele la Bwana kila mara unapokuwa katika Kuomba, waombee watoto wako mema mbele za Bwana kama vile mama yao mtume Yakobo na Yohana alivyofanya.Mbali na hilo, jambo lingine ni kwenda na mtoto ibadani, kwasababu, katika ibada pia, malaika wa Bwana hujiudhulisha kwa wingi sana kwa lengo la kuwahudumia watakatifu, hivyo wanaposhuka kwa lengo hilo mtoto nae atakuwa ni sehemu ya hao watakao hudumiwa.

Waebrania 1:13-14 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?.

3. Mwimbie/Mfundishe nyimbo za Injili, sifa, kuabudu na tenzi za rohoni

Katika vitu vya msingi na vya kuzingatia pia ni hapa, kwasababu maneno ni roho, hivyo, kamwe mzazi usiruhusu kumfundisha na kumzoesha mwanao kusikiliza miziki ya kidunia, au mtu awe anamwimbia miziki ya kidunia iliyojaa uzinzi ndani yake na matusi ya namna mbali mbali, kwani kwa kufanya hivyo, utakuwa unapanda mbegu ya shetani ndani yake, bali mwimbie nyimbo za injili, sifa, au tenzi za rohoni ili kumfanya akili yake imjue Mungu zaidi kuliko vitu vingine katika hali hiyo hiyo ya uchanga na utoto aliyo nayo, na kwa nyimbo hizo, Yesu Kristo atazidi kujaa ndani yake katika umri huo huo alionao na utakua umepanda mbegu njema ndani yake na kwako utakuwa umetimiza neno linalosema.

Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

service-image

Tunawalea Kimaadili

Watoto

Tunawahamasisha Elimu

Watoto

service-image

Kulea watoto kimaadili

Kanisa ni Tasisi inayougana na Serikali katika Kulea watoto kimaadili, Tag Shekinah tumekuwa tukijihusisha na Kulea watoto katika nyanja za Maadili, Utumishi na Ustaarabu.

Learn more
service-image

Kusaidia watoto wenye Uhitaji

Tag shekinah tumekuwa tukijihusisha moja kwa moja na kusaidia watoto wanaotoka Jamii zenye uchumi mdogo ambapo mahitaji muhimu kwao ni changamoto kama chakula, Mavazi na Mahitaji ya shule.

Learn more
service-image

Kuhamasisha Kuhusu Elimu

Tumekuwa tukiwahamasisha na kuwaelimisha watoto kujitambua na kuelewa umuhimu wa Elimu, Kuelimika ni mpango wa Mungu, Hivyo watoto wetu wakisoma watapata Maendeleo.

Learn more