Who We Are
Tag Shekinah ni kanisa la Kipentekoste ambalo ni Tawi la Tanzania Assemblies of God (TAG) linaloendesha huduma za kiroho likijikita kwenye Mambo makubwa kama Kuhubiri Injili ya kweli kwa watu wote ili wamjue Mungu na kuacha uovu, kuelimisha jamii kimaadili,kufanya huduma za ufungulivu kwa wanaoteseka, kufanya miradi ili kuigusa Jamii na Kuungana na Serikali katika harakati mbali mbali za maendeleo.
Mchungaji Stephen Peter Mhina Anaamini kwamba, Mkristo akishafundishwa juu ya Imani ya Mungu wa kweli, ataweza kunufaika na baraka za Mungu ipasavyo na ataweza kujitegemea na kuwa Imara katika Maisha yake ya utumishi na Jamii yake. Mkristo Imara katika Imani ndiyo chachu ya Ibada zenye nguvu. Hapa ndipo ndipo tutaweza kufanikiwa kuhubiri Injili duniani yenye mafanikio. "Marko 16:15-16 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa".
Tag Shekina Church hutekeleza maono makubwa chini ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God ambao huamini katika Misingi 16 katika kuhubiri neno la Mungu la kweli kutapelekea kuwa na waumini wenye kumjua Mungu kikamilifu na hawa ndio wataweza kumtumikia Mungu katika kicho chake, wataishi maisha matakatifu, Watakuwa ni mabalozi wazuri wa kuhubiri Injili ya kweli na mwisho ni kuwa na kanisa lenye Nguvu za Mungu litakaloweza kuyashinda malango ya kuzimu na kuathiri Jamii kwa maendeleo. "Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia".
Shekinah Intercessory Temple